Sunday, July 14, 2013

NJIA SALAMA ZA KUPUNGUZA UNENE

KIRIBATUMBO NI NINI?

Chakula tunachokula huwa kinatumika mwilini ili kuupa mwili nguvu pamoja na kufanya kazi zingine muhimu mwilini
Ila chakula hicho hakiwezi kutumika chote kwa wakati mmoja na hivyo kingine kinageuzwa na ini kua mafuta na kisha kuhifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya baadae. 
Mafuta hayo yanapozidi mwilini huleta madhara na kusababisha kiribatumbo (obesity)
kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kiteknolojia imekua ni jambo la kawaida kwa watu wengi kuwa na unene uliopita kiasi (obese)


MADHARA YA UNENE ULIOPITA KIASI
Unene uliopita kiasi una madhara mengi kiafya, kijamii na hata kiuchumi.baadhi ya madhara yanayoweza kusababishwa na unene uliopitiliza ni pamoja na:
 • Shinikizo la damu
 • Matatizo ya moyo (heart failure)
 • Kisukari
 • kiarusi (stroke)
 • Matatizo ya kizazi (infertility)
 • Kuongeza hatari ya kupata kansa ya kizazi kwa wanaume (prostate cancer)
 • Kukoroma kupita kiasi wakati wa kulala
 • Watoto wanene kupita kiasi huonewa shuleni na hivyo kushindwa kufanya vizuri darasani


VISABABISHI VYA UNENE
Kuna mambo mengi yanayoweza kuchangia mtu akawa mnene, ila sababu nyingi husababishwa na mtindo wa maisha ikiwemo vyakula tunavyokula. Sababu hizo ni pamoja na:
 • Kula vyakula vingi vyenye sukari
 • Kutokufanya mazoezi
 • Kula vyakula vingi vyenye wanga
 • Kurithi
UTAJUAJE KWAMBA UNA UNENE ULIOPITILIZA?
hupimwa kwa kutumia body mass index calculator unachotakiwa kufanya ni kujua uzito wako pamoja na urefu wako.
                                     JINSI YA KUTUMIA BODY MASS INDEX CALCULATOR
1. Kwanza kabisa pima uzito wako kwa kutumia mizani ya kupimia uzito. Mizani za kupimia uzito hupatikana sehemu mbalimbali kama vile kwenye vituo vya afya, maduka ya dawa na hata sehemu nyingine zozote.
-Baada ya kupima weka kumbukumbu ya uzito wako kwa kuandika mahali

2. Pima urefu wako (kwa kizio cha sentimita)

Kwa kutumia body mass  index calculator fuata maelekezo na ujaze uzito pamoja na urefu wako kulingana na jinsi ulivyopima (anza kwa kubonyeza kitufe kilichoandikwa "metric"
 • Ukipata jibu chini ya 18, uzito wako ni mdogo kupita kiasi
 • Ukipata 18.6-24.6,ni uzito wa mtu mwenye afya nzuri
 • Ukipata 25-29.9, ni uzito uliopitiliza
 • Ukipata 30, ni unene kupita kiasi (kiribatumbo/obesity)

JINSI YA KUPUNGUZA UNENE ULIOPITILIZA
Unaweza kupunguza unene kwa kutumia njia zifuatazo:
 • Fanya mazoezi mara kwa mara
 • Kula mbogamboga na matunda kwa wingi
 • Epuka matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi
 • Kula nafaka ambazo hazijakobolewa (mfano: unga wa dona)
 • Kula mbogamboga na matunda kwa wingi
 •  Tumia vyakula vyenye calcium kwa wingi
 • Kwa wanaofanya kazi maofisini, punguza kula vyakula vya wanga

NB: Ifahamike kwamba, kupunguza unene haimaanishi kuwa mtu anatakiwa kupunguza kula ila tu ni kula chakula bora

vyanzo: bbc.com/heaalth
              Center for disease control (CDC)

No comments:

Post a Comment