Thursday, June 26, 2014

HOMA YA MANJANO

Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi viitwavyo flavivirus. Ugonjwa huu huenezwa na mbu aina ya aedes aegypti na ni vigumu kuutofautisha na magonjwa mengine kama malaria kwenye dalili za mwanzo bila kutumia vipimo. Ugonjwa huu hushambulia seli za kinga mwilini (macrophages, monocytes). 
Baada ya kuingia ndani ya seli, virusi vya homa ya manjano huzaliana na kuendelea kukua huku wakihama kutoka kwenye seli moja hadi nyingine kushambulia. Virusi huenda kwenye seli za ini na kuanza kuzishambulia na hivyo kusababisha sumu kwenye damu

DALILI ZA HOMA YA MANJANO
Baada ya kuambukizwa homa ya manjano, huchukua siku tatu hadi sita kabla ya dalili za mwanzo kuanza kujitokeza. Dalili za mwanzo za homa ya manjano ni pamoja na:

  • Homa 
  • Maumivu ya kichwa
  • Maumivu ya mgongo
  • Kukosa hamu ya kula (anorexia)
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Uchovu na udhaifu wa mwili






Asilimia 15 ya watu wanaopata homa ya manjano huingia kwenye hatua ya pili ya ugonjwa huu, isababishwayo na kuharibika kwa ini. Hatua ya pili  inaambatana na dalili mbaya zaidi zikiwemo:

  • Jaundice (macho, ulimi na viganja kubadilika kuwa rangi ya njano)
  • Maumivu makali ya tumbo
  • Kutapika damu
  • Kutokwa na damu machoni na mdomoni (hemorrhage)
Mgonjwa akifanikiwa kupona ugonjwa huu, atakua amejijengea kinga hivyo hataweza kupata homa ya manjano maisha yake yote.



CHANJO

Chanjo ya homa ya manjano ijulikanayo kama YF-VAX® 17D inapatikana na hutotolewa kila mwaka
kwenye vituo vya afya kwa watu wote, ikiwemo wasafiri na watalii watokao nchi za nje.

MATIBABU


Matibabu ya uhakika ya homa ya manjano  hayajapatikana, kutokana na ukweli kwamba ugonjwa huu unasababishwa na virusi na hivyo hakuna dawa inayoaminika kwamba itaweza kuua kabisa virusi hivi, hivyo ni vyema kupata chanjo ya homa ya manjano kabla hujapatwa na ugonjwa wenyewe.
Wizara ya afya hutoa chanjo ya homa ya manjano kwa watoto walio chini ya miaka mitano kila mwaka hivyo ni vyema umpeleke mtoto wako siku itakapotangazwa

JINSI UGONJWA UNAVYOSAMBAZWA

Ugonjwa wa homa ya manjano huenezwa na mbu aina ya aedes, ambaye hupatikana katika maeneo ya  katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara, ikiwemo Tanzania. Mbu jike aina ya aedes hupendelea kunyonya damu pindi awapo mjamzito ili kumwezesha kurutubisha mayai yake. Mbu aliyenyonya damu ya mtu mwenye homa ya manjano huweza kumwambukiza mtu mwingine.
kitropik na savanna, ikiwemo Afrika, amerika ya kusini pamoja na mashariki ya mbali. Mbu hawa kwa Afrika hupatikana zaidi
Ugonjwa huu pia huweza kuenezwa kwa kuchangia sindano na mtu ambaye tayari ameambukizwa ugonjwa wa homa ya manjano na pia kuwekewa damu au kupandikizwa kiungo cha  mtu aliyeathirika kunaweza kusababisha maambukizi.
   

NJIA ZA KUJIKINGA NA HOMA YA MANJANO
Mbinu za kujikinga na homa ya manjano zinahusisha kujikinga kuumwa na mbu, na nyingi zinafanana na zile za kujikinga na malaria pamoja na dengue fever. Zifuatazo ni baadhi ya njia za kujikinga na homa ya manjano
:
  • Vaa nguo ndefu zinazofunika mwili vizuri
  •  Pulizia dawa ya mbu kwenye nyumba ili kuua mbu
  •  Tokomeza mazalia ya mbu kwa kufukia maji yaliyotuama, ikiwa na pamoja na makopo, vifuu pamoja na vitu vingine vinavyoweza kukinga maji.
  • Mtu akigundulika kwamba ana homa ya manjano atibiwe haraka ili kuzuia ugonjwa kusambaa
  • Usichangie sindano pamoja na watu wengine, kwani kuna hatari ya kuambukizwa magonjwa mengi ikiwemo homa ya manjano




Vyanzo

No comments:

Post a Comment