Tuesday, July 16, 2013

USIYOYAFAHAMU KUHUSU SHINIKIZO LA DAMU (Hypertension/high bloodpressure)


Reviewed by: Dr. Chaula Nezaron
                     +255753095035

SHINIKIZO LA DAMU NI NINI?

Ni ugonjwa unaosababisha kuongezeka kwa msukumo wa damu kwenye mishipa inayotoa damukwenye moyo (arteries). Shinikizo la damu ni mojawapo kati ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Ugonjwa huu husababisha  moyo kufanya kazi kwa nguvu Zaidi ya kawaida ili kusukuma damu mwilini. Tatizo la msongo wa damu, pamoja kisukari ni matatizo ambayo yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mtindo wa maisha, na idadi ya watu wanaougua ugonjwa huu imekua ikiongezeka siku hadi siku kutokana na mabadiliko hayo.
Ugonjwa huu ni hatari kwa kuwa mara nyingi hauonyeshi dalili zozote, mpaka mtu anapoanza kuathirika kwa kiasi kikubwa (chronic)

AINA ZA SHINIKIZO LA DAMU (Presha)


  Primary hypertension

Hii ni aina ya presha inayowakumba watu wengi (90-95%) kuliko aina nyingine ya shinikizo la damu, na huwa sababu zinazopelekea aina hii ya shinikizo la damu hazijulikani mpaka sasa.
2    
              Secondary hypertension

Hii ni aina ya shinikizo la damu linalokumba asilimia chache Zaidi (5-10%) ya watu kuliko aina ya kwanza ya shinikizo la damu. Aina hii ya shinikizo la damu unaweza kusababishwa na matatizo kama:
·         Watu watokao kwenye familia zenye historia ya kupata shinikizo la damu wana hatari kubwa Zaidi ya kupata shinikizo la damu kuliko watu watokao kwenye familia zisizo na historia hiyo.

  •  Matatizo ya moyo (Heart failure)


  • Matatizo ya figo (Renal failure)


  •  Matatizo ya mishipa ya damu ( kupungua ukubwa wa mishipa ya damu/atherosclerosis)


  • Unene kupita kiasi (Obesity)


  • Watu wasiofanya mazoezi mara kwa mara wana hatari kubwa Zaidi ya kupata shinikizo la damu

  •  Kutumia chumvi nyingi

  •  Ulevi wa pombe, sigara na dawa za kulevya

  • Magonjwa ya meno


  • ·     Watu wenye umri kati ya miaka 40 na kuendelea wana uwezekano mkubwa Zaidi wa kupata shinikizo la damu.

  

  
Shinikizo la damu wakati wa ujauzito
Imegundulika kwamba asilimia 8-10% ya akina mama wanapata shinikizo la damu wakati wa ujauzito na huchangia asilimia 16% ya vifo vya wajawazito duniani pamoja na kuongeza hatari ya vifo vya watoto wachanga kabla ya kujifungua na hivyo akina mama wanashauriwa wahudhurie kliniki ili wafahamu njia za kujikingA
Wajawazito wenye shinikizo la damu huwa wanaweza wakapata dalili zifuatazo:
  •  Kushindwa kuona vizuri
  •   Kujaa maji kwenye mapafu (pulmonary edema)
  • Miguu kujaa maji ( edema)
  •  Kizunguzungu

SHINIKIZO LA DAMU KWA WATOTO
Dalili za shinikizo la damu kwa watoto
  
  •  Kutokwa na damu puani
·  Matatizo ya macho
·  Mtoto kushindwa kukua vizuri
·  Paralysis

Visababishi vya shinikizo la damu kwa watoto
Watoto wanaweza kupata shinikizo la damu kutokana na sababu zifwatazo:
  • Matumizi ya pombe na sigara wakati wa ujauzito
  •   Kuzaliwa kabla ya siku (premature birth)
  •   Kukosa maziwa ya mama (kutokunyonyesha)

  
JINSI YA KUJIKINGA NA SHINIKIZO LA DAMU
  • Fanya mazoezi mara kawa mara
  •  Punguza matumizi ya chumvi na sukari
  •  Punguza matumizi ya pombe
  •  Kula matunda na mboga mboga kwa wingi
  • Epuka vyakula vyenye mafuta mengi

N.B: Kwa kua mara nyingi kisukari hakina dalili kwa watu wazima, ni muhimu kuhudhuria kwenye kituo cha afya mara kwa mara ili ukapime shinikizo la damu

Kwa akina mama wajawazito:

  •  Epuka pombe na sigara wakati wa ujauzito
  •    Fanya mazoezi mepesi ya mwili wakati wa ujauzito

  •   Hakikisha mtoto anapata maziwa ya mama, na wala siyo maziwa ya makopo

  •   Hudhuria kliniki kipindi chote cha ujauzito kama unavyoelekezwa na wahudumu wa afya.
  • Kama una matatizo ya meno, mwone daktari utibiwe mapema kwani yanaweza kusababisha matatizo ya moyo







MATIBABU


Matibabu ya shinikizo la damu bado hayajapatikana,  lakini dawa za kutuliza zinapatikanatembelea kituo cha afya kilicho karibu nawe kwa ushauri Zaidi.

vyanzo:



















No comments:

Post a Comment