Friday, May 23, 2014

HOMA YA DENGUE


     Huu ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya dengue (dengue virus) na kusambazwa na mbu aina ya aedes. Mpaka sasa ugonjwa wa dengue hauna kinga. Ugonjwa wa dengu unapatikana Zaidi katika maeneo yenye joto (tropical regions) ambayo mengi yapo karibu na ikweta. Katika miaka ya karibuni maambukizi ya ugonjwa huu yameongezeka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, muongezeko wa idadi ya watu pamoja na kuongezeka kwa safari za nje ya nchi Ugonjwa wa dengue umeenea Zaidi katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara, amerika ya kusini pamoja na asia ya kusini.


JINSI UGONJWA UNAVYOSAMBAZWA

Ugonjwa wa dengue husambazwa na mbu aina ya aedes ambao hupendelea kuishi na kuzaliana kwenye maji yaliyotuama na mbu hawa hupendelea kuuma nyakati za mchana. Mbu huweza kusamabaza ugonjwa wa dengu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Ugonjwa huu pia unawezwa kusambazwa kwa njia  ya kuongezewa damu ya mtu mwenye dengue, au kwa kubadilishiwa kiungo cha mtu mwenye dengue (mfano figo)


DALILI ZA HOMA YA DENGUE

Zaidi ya asilimia 80 ya watu walioambukizwa dengue huwa hawaonyeshi dalili zozote za ugonjwa huu.
Dalili za ugonjwa wa dengu kwa wastani hujitokeza siku 3 hadi siku 14 baada ya kuambukizwa, ila kwa watu walio wengi dalili hujitokeza siku 4 hadi 7 baada ya kuumwa na mbu mwenye ugonjwa huu.
Dalili za mwanzo za dengue ni pamoja na:
  • ·         Homa
  • ·         Kuharisha na kutapika
  • ·         Mumivu makali ya kichwa
  • ·         Maumivu ya misuli na viungo
  • ·         Uchovu wa mwili

Ugonjwa usipotibiwa mapema Baatdi ya watu pia huweza kupata dalili ,baya Zaidi kama vile:
  • ·         Kutokwa na damu kwenye sehemu zenye uwazi(puani, mdomoni)
  • ·         Kupungu kazi ya mapigo ya moyo
  • ·         Kupata vipele vyekundu kwenye ngozi (erythema)
  • ·         Damu kushindwa kuganda likitokea jeraha

Ugonjwa wa dengue pia huweza kupeleka matatizo ya moyo, upungufu wa damu pamoja na matatizo ya ini
Ni rahisi kuzifananisha dalili nyingi za homa ya dengu na zile za malaria pamoja na mafua hivyo ni vyema ukapime kwanza kabla hujaanza matibabu ya malaria.  

MATIBABU
Tiba ya dengue inalenga kupunguza dalili za ugonjwa na wala siyo kuangamiza virus vya dengue (symptomatic treatment). Dawa ya maumivu inayoshauriwa kutumika kutuliza maumivu kwa wenye ugonjwa huu ni PARACETAMOL.
Utafiti uliofanyika nchini India na kuchapishwa kwenye tovuti ya wizara ya afya ya marekani, umethibitisha kwamba majani ya mpapai (carica papaya) yana uwezo wa kutibu ugonjwa wa dengue. Hata hivyo, Dk Vinitah Saini kutoka hospitali ya Muhimbili alisema ingawa baadhi ya maeneo wanatumia juisi ya majani ya mpapai kutibu ugonjwa huo lakini akasema hakuna ushahidi wa kisayansi  kuwa yanatibu. Majani hayo hutumika kutengeneza juisi ambayo hunywewa kama dawa

TAHADHARI
Matumizi ya dawa za maumivu kama vile ASPIRIN na IBUPROFEN ni hatari kwa mtu mwenye homa ya dengue kwani zinaweza kufanya hali iwe mbaya Zaidi na kusababisha kifo. Dawa za aspirini pamoja na ibuprofen husababisha damu nyingi Zaidi kuvuja na hivyo hupelekea upungufu mkubwa Zaidi wa damu.

JINSI YA KUJIKINGA NA HOMA YA DENGUE
Mbinu za kujikinga na dengue zinahusisha kujikinga kuumwa na mbu, na nyingi zinafanana na zile za kujikinga na malaria. Zifuatazo ni baadhi ya njia za kujikinga na homa ya dengue:

  •          Vaa nguo ndefu zinazofunika mwili vizuri

  •          Pulizia dawa ya mbu kwenye nyumba ili kuua mbu
  •          Tokomeza mazalia ya mbu kwa kufukia maji yaliyotuama, ikiwa na pamoja na makopo, vifuu pamoja na vitu vingine vinavyoweza kukinga maji.

  •                                                  ·   Lala kwenye chandarua
  •     Jipake mafuta ya kufukuza mbu

Vyanzo:

No comments:

Post a Comment