Thursday, June 26, 2014

HOMA YA MANJANO

Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi viitwavyo flavivirus. Ugonjwa huu huenezwa na mbu aina ya aedes aegypti na ni vigumu kuutofautisha na magonjwa mengine kama malaria kwenye dalili za mwanzo bila kutumia vipimo. Ugonjwa huu hushambulia seli za kinga mwilini (macrophages, monocytes). 
Baada ya kuingia ndani ya seli, virusi vya homa ya manjano huzaliana na kuendelea kukua huku wakihama kutoka kwenye seli moja hadi nyingine kushambulia. Virusi huenda kwenye seli za ini na kuanza kuzishambulia na hivyo kusababisha sumu kwenye damu

DALILI ZA HOMA YA MANJANO
Baada ya kuambukizwa homa ya manjano, huchukua siku tatu hadi sita kabla ya dalili za mwanzo kuanza kujitokeza. Dalili za mwanzo za homa ya manjano ni pamoja na:

  • Homa 
  • Maumivu ya kichwa
  • Maumivu ya mgongo
  • Kukosa hamu ya kula (anorexia)
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Uchovu na udhaifu wa mwili






Asilimia 15 ya watu wanaopata homa ya manjano huingia kwenye hatua ya pili ya ugonjwa huu, isababishwayo na kuharibika kwa ini. Hatua ya pili  inaambatana na dalili mbaya zaidi zikiwemo:

  • Jaundice (macho, ulimi na viganja kubadilika kuwa rangi ya njano)
  • Maumivu makali ya tumbo
  • Kutapika damu
  • Kutokwa na damu machoni na mdomoni (hemorrhage)
Mgonjwa akifanikiwa kupona ugonjwa huu, atakua amejijengea kinga hivyo hataweza kupata homa ya manjano maisha yake yote.



CHANJO

Chanjo ya homa ya manjano ijulikanayo kama YF-VAX® 17D inapatikana na hutotolewa kila mwaka
kwenye vituo vya afya kwa watu wote, ikiwemo wasafiri na watalii watokao nchi za nje.

MATIBABU


Matibabu ya uhakika ya homa ya manjano  hayajapatikana, kutokana na ukweli kwamba ugonjwa huu unasababishwa na virusi na hivyo hakuna dawa inayoaminika kwamba itaweza kuua kabisa virusi hivi, hivyo ni vyema kupata chanjo ya homa ya manjano kabla hujapatwa na ugonjwa wenyewe.
Wizara ya afya hutoa chanjo ya homa ya manjano kwa watoto walio chini ya miaka mitano kila mwaka hivyo ni vyema umpeleke mtoto wako siku itakapotangazwa

JINSI UGONJWA UNAVYOSAMBAZWA

Ugonjwa wa homa ya manjano huenezwa na mbu aina ya aedes, ambaye hupatikana katika maeneo ya  katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara, ikiwemo Tanzania. Mbu jike aina ya aedes hupendelea kunyonya damu pindi awapo mjamzito ili kumwezesha kurutubisha mayai yake. Mbu aliyenyonya damu ya mtu mwenye homa ya manjano huweza kumwambukiza mtu mwingine.
kitropik na savanna, ikiwemo Afrika, amerika ya kusini pamoja na mashariki ya mbali. Mbu hawa kwa Afrika hupatikana zaidi
Ugonjwa huu pia huweza kuenezwa kwa kuchangia sindano na mtu ambaye tayari ameambukizwa ugonjwa wa homa ya manjano na pia kuwekewa damu au kupandikizwa kiungo cha  mtu aliyeathirika kunaweza kusababisha maambukizi.
   

NJIA ZA KUJIKINGA NA HOMA YA MANJANO
Mbinu za kujikinga na homa ya manjano zinahusisha kujikinga kuumwa na mbu, na nyingi zinafanana na zile za kujikinga na malaria pamoja na dengue fever. Zifuatazo ni baadhi ya njia za kujikinga na homa ya manjano
:
  • Vaa nguo ndefu zinazofunika mwili vizuri
  •  Pulizia dawa ya mbu kwenye nyumba ili kuua mbu
  •  Tokomeza mazalia ya mbu kwa kufukia maji yaliyotuama, ikiwa na pamoja na makopo, vifuu pamoja na vitu vingine vinavyoweza kukinga maji.
  • Mtu akigundulika kwamba ana homa ya manjano atibiwe haraka ili kuzuia ugonjwa kusambaa
  • Usichangie sindano pamoja na watu wengine, kwani kuna hatari ya kuambukizwa magonjwa mengi ikiwemo homa ya manjano




Vyanzo

Friday, May 23, 2014

HOMA YA DENGUE


     Huu ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya dengue (dengue virus) na kusambazwa na mbu aina ya aedes. Mpaka sasa ugonjwa wa dengue hauna kinga. Ugonjwa wa dengu unapatikana Zaidi katika maeneo yenye joto (tropical regions) ambayo mengi yapo karibu na ikweta. Katika miaka ya karibuni maambukizi ya ugonjwa huu yameongezeka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, muongezeko wa idadi ya watu pamoja na kuongezeka kwa safari za nje ya nchi Ugonjwa wa dengue umeenea Zaidi katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara, amerika ya kusini pamoja na asia ya kusini.


JINSI UGONJWA UNAVYOSAMBAZWA

Ugonjwa wa dengue husambazwa na mbu aina ya aedes ambao hupendelea kuishi na kuzaliana kwenye maji yaliyotuama na mbu hawa hupendelea kuuma nyakati za mchana. Mbu huweza kusamabaza ugonjwa wa dengu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Ugonjwa huu pia unawezwa kusambazwa kwa njia  ya kuongezewa damu ya mtu mwenye dengue, au kwa kubadilishiwa kiungo cha mtu mwenye dengue (mfano figo)


DALILI ZA HOMA YA DENGUE

Zaidi ya asilimia 80 ya watu walioambukizwa dengue huwa hawaonyeshi dalili zozote za ugonjwa huu.
Dalili za ugonjwa wa dengu kwa wastani hujitokeza siku 3 hadi siku 14 baada ya kuambukizwa, ila kwa watu walio wengi dalili hujitokeza siku 4 hadi 7 baada ya kuumwa na mbu mwenye ugonjwa huu.
Dalili za mwanzo za dengue ni pamoja na:
  • ·         Homa
  • ·         Kuharisha na kutapika
  • ·         Mumivu makali ya kichwa
  • ·         Maumivu ya misuli na viungo
  • ·         Uchovu wa mwili

Ugonjwa usipotibiwa mapema Baatdi ya watu pia huweza kupata dalili ,baya Zaidi kama vile:
  • ·         Kutokwa na damu kwenye sehemu zenye uwazi(puani, mdomoni)
  • ·         Kupungu kazi ya mapigo ya moyo
  • ·         Kupata vipele vyekundu kwenye ngozi (erythema)
  • ·         Damu kushindwa kuganda likitokea jeraha

Ugonjwa wa dengue pia huweza kupeleka matatizo ya moyo, upungufu wa damu pamoja na matatizo ya ini
Ni rahisi kuzifananisha dalili nyingi za homa ya dengu na zile za malaria pamoja na mafua hivyo ni vyema ukapime kwanza kabla hujaanza matibabu ya malaria.  

MATIBABU
Tiba ya dengue inalenga kupunguza dalili za ugonjwa na wala siyo kuangamiza virus vya dengue (symptomatic treatment). Dawa ya maumivu inayoshauriwa kutumika kutuliza maumivu kwa wenye ugonjwa huu ni PARACETAMOL.
Utafiti uliofanyika nchini India na kuchapishwa kwenye tovuti ya wizara ya afya ya marekani, umethibitisha kwamba majani ya mpapai (carica papaya) yana uwezo wa kutibu ugonjwa wa dengue. Hata hivyo, Dk Vinitah Saini kutoka hospitali ya Muhimbili alisema ingawa baadhi ya maeneo wanatumia juisi ya majani ya mpapai kutibu ugonjwa huo lakini akasema hakuna ushahidi wa kisayansi  kuwa yanatibu. Majani hayo hutumika kutengeneza juisi ambayo hunywewa kama dawa

TAHADHARI
Matumizi ya dawa za maumivu kama vile ASPIRIN na IBUPROFEN ni hatari kwa mtu mwenye homa ya dengue kwani zinaweza kufanya hali iwe mbaya Zaidi na kusababisha kifo. Dawa za aspirini pamoja na ibuprofen husababisha damu nyingi Zaidi kuvuja na hivyo hupelekea upungufu mkubwa Zaidi wa damu.

JINSI YA KUJIKINGA NA HOMA YA DENGUE
Mbinu za kujikinga na dengue zinahusisha kujikinga kuumwa na mbu, na nyingi zinafanana na zile za kujikinga na malaria. Zifuatazo ni baadhi ya njia za kujikinga na homa ya dengue:

  •          Vaa nguo ndefu zinazofunika mwili vizuri

  •          Pulizia dawa ya mbu kwenye nyumba ili kuua mbu
  •          Tokomeza mazalia ya mbu kwa kufukia maji yaliyotuama, ikiwa na pamoja na makopo, vifuu pamoja na vitu vingine vinavyoweza kukinga maji.

  •                                                  ·   Lala kwenye chandarua
  •     Jipake mafuta ya kufukuza mbu

Vyanzo:

Sunday, January 19, 2014

MATUMIZI SALAMA YA ASPIRIN

Aspirin ni dawa inayotumika kutuliza maumivu na uvimbe(inflammation)  katika mwili. Dawa hii pia hutumika kutuliza homa pamoja na  kuzuia matatizo ya moyo(atherosclerotic plaque), saratani ya utumbo mpanana(colorectal cancer),  kiharusi endapo daktari ataona ni vema. Aspirin hutumika kutuliza maumivu ya kichwa, mgongo,meno, misuli na mengine yanayofanana na hayo. madhara(side effects) za aspirin zinatofautiana kulingana na umri, hali ya kiafya pamoja na kiasi cha dawa kilichotumika.
1. WATOTO
Aspirini haishauriwi kutumika na watoto wadogo kwani zinaweza kusababisha ugonjwa uitwao Reye's syndrome. Ugojwa huu mara nyingi huwapata watoto wenye umri chini ya miaka 12 ambao wanatumia aspirin mara kwa mara. Imegundulika kwamba watoto wenye magonjwa kama tetekuwanga wana hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa huu baada ya kutumia aspirin. Ugonjwa huu hushambulia ini na ubongo na unaweza kusababisha kifo kama mtoto hatapata matibabu haraka.

Dalili za Reye's syndrome ni pamoja na:
  • Kutapika mara kwa mara
  • Mabadiliko ya tabia
  • Kuzubaa
  • Kupumua haraka haraka(hyperventilation)
Dalili hizi hutokea baada  tu ya kupona ugonjwa wa mafua au tetekuwanga.
Uwepo wa ugonjwa huu unaweza kugundulika kwa kupimwa damu au mkojo na matibabu ya haraka yanahitajika ili kuzuia madhara makubwa zaidi kwenye ubongo pamoja na ini ambayo yanaweza kusababisha kifo. 

2. VIDONDA VYA TUMBO(ulcers)
Inashauriwa watu wenye vidonda vya tumbo wasitumie Aspirin kwani inaweza kuongeza tatizo hilo na hata kusababisha uvujaji wa damu tumboni. Dawa mbadala kama vile paracetamol inaweza ikatumika kutuliza maumivu badala ya aspirin kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo kwa kuwa aspirin ina asili ya tindikali(acidic). 

3. KIUNGULIA(heart burn)
Kwa kuwa aspirin huongeza kiasi cha tindikali tumboni, kiasi kidogo cha tindikali hiyo hurudi kwenye koo la chakula na kusababisha mtu apate kiungulia.

4. KUVUJA DAMU KWENYE UBONGO(Cerebral hemorrhage)
 Moja wapo kati ya kazi za aspirin ni kuzuia damu kuganda(anti-clotting) na hivyo huweza kusababisha kuvuja kwa damu kwenye ubongo.
  • Watu wanaotarajia kufanyiwa upasuaji wanashauriwa wasitumie aspirin kwa kuwa inaweza ikasababisha wavuje damu nyingi wakati wa upasuaji.
5. ALEJI (allergy)
Baadhi ya watu hupata madhara baada ya kutumia aspirin. Baadhi ya dalili za kuwa na aleji ya aspirin hutokea lisaa limoja baada ya kumeza kidonge cha aspirin nazo ni ni pamoja na:
  • Kuwashwa kwa ngozi pamoja na kutokwa na vipele(skin rashes)
  • Kushindwa kupumua vizuri(pumu/asthma)  
 6. KUTUMIA KIASI KIKUBWA CHA ASPIRIN (aspirin poisoning/salycilism)
 Kama zilivyo dawa zingine, matumizi makubwa ya dawa hii huifanya iwe sumu mwilini(intoxication). Sumu zilizoko mwilini huchujwa kwenye ini ila, ini huzidiwa kama kiasi cha sumu kikizidi. Matumizi ya aspirin kwa muda mrefu pia huweza kusababisha magonjwa ya ini pamoja na figo. Dalili zake hutegemea na kiasi pamoja na muda wa matumizi, 
Madhara yatokanayo na matumizi ya kiasi kikubwa cha aspirin kwa muda mfupi(Acute aspirin poisoning )
  • Maumivu makali ya tumbo
  • Kichefuchefu na kutapika
Madhara yatokanayo na matumizi ya kiasi  kidogo cha aspirin kwa muda mrefu(Chronic aspirin poisoning )
  • Uchovu
  • Kutetemeka(seisures)
  • Moyo kwenda mbio
  • Kupumua kwa kasi(hyperventilation)
MUINGILIANO NA DAWA NYINGINE
  • Kwa wanaotumia dawa za kisukari, aspirin inaweza ikasababisha sukari kushuka kupita kiasi (hypoglycemia) 
  • Kwa wanaotumia aspirin ili kuzuia matatizo ya moyo au kiharusi, hawatakiwi wachanganye pamoja na dawa zingine za maumivu kama ibuprofen
  • Madhara ya aspirin huongezeka pale inaponywewa pamoja na pombe, kwani husababisha damu kuvuja kwa wingi tumboni kwa watu wenye vidonda vya tumbo
MATUMIZI SALAMA YA ASPIRIN
  • Ili kupunguza hatari ya kupata vidonda vya tumbo, usitafune aspirin, meza kama ilivyo.
  • Meza aspirin kwa angalau glass moja ya maji
  • Usivunje wala kusaga kidonge cha aspirin kabla ya kumeza
  • Hakikisha unamtaarifu daktari wako kama unatumia aspirin kabla ya upasuaji/operesheni(surgery)
  • Watoto wa chini ya miaka 12 wasitumia aspirin pasipo ushauri wa daktari
  • Usitumie vidonge vya aspirin vyenye harufu ya siki(vinegar) kwani vinaashiria kuwa vimeisha muda wake
SOURCES

Saturday, October 19, 2013

MAAJABU YA MWILI WA BINADAMU

1.Joto linalozalishwa na mwili wa binadamu kwa muda wa nusu saa linatosha kufanya nusu galoni la maji lichemke! Hii inamaanisha kwamba joto la mwili linaweza kuchemsha galoni zima la maji kwa lisaa limoja.
















2.Inakadiriwa kwamba mtu wa kawaida mwenye miaka 70 huwa tayari ametengeneza galoni 6250 za MATE katika maisha yake. Kiasi hicho kinatosha kujaza mabwawa mawili ya kuogelea! (swimming pools)




















3. Mishipa iliyoko mwilini kwa mtu mzima ikiunganishwa pamoja inaweza kufikia urefu wa maili elfu sitini (60,000) au kilomita 96,560. Kwa urefu huo mishipa ya binadamu mmoja inawaza ikaizunguka dunia mara mbili, kwani mzingo wa dunia ni kilomita 40,075!
























4. Moyo wa binadamu husukuma lita 445 za damu kila siku, Hizo ni sawa na ndoo kubwa 23 za maji
























5. Tindikali inayozalishwa kwenye tumbo la binadamu ina uwezo wa kuyeyusha viwembe





6. Binadamu hawezi kupiga chafya akiwa amefungua macho

7. Kusikiliza muziki baada ya kula kunasaidia mmeng'enyo wa chakula (digestion) ufanyike kwa ufanisi zaidi


8. Kukosa usingizi kunachangia mtu kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara. Hii ni kwa sababu usingizi ni muhimu katika kutengeneza kinga ya mwili

9. Kwa kawaida tumbo la binadamu hutengeneza lita 2 za tindikali (Hydrochloric acid) kwa siku

10. Imegundulika kwamba kucheka ni dawa nzuri ya maumivu (painkiller)




11. Mtu hutumia misuli 200 kupiga hatua moja anapotembea. Hii inajumuisha misuli ya miguu pamoja na mikono.


12. watoto wana mifupa mingi kuliko watu wazima. Watoto wana mifupa 300 wakati watu wazima wana mifupa 206. Hii inatokana na kwamba baadhi ya mifupa ya watoto huungana pamoja wakati anapoelekea utu uzima.

13. Binadamu anapofikisha miaka 18 chembe hai (seli) zake za ubongo huacha kukua na badala yake huanza kufa. 

Friday, August 2, 2013

UNAJUA NINI KUHUSU ANTIOXIDANTS?


Reviewed by; Dr. Chaula Nezaron
                     +255753095035

KWANINI TUTUMIE VYAKULA VYENYE ANTIOXIDANTS?



Seli za mwili huitaji hewa ya oksijen ili ziweze kufanya kazi. Hewa ya oksijen hutumika kuunguza vyakula tunavyokula ili kuupatia mwili nguvu. Ili hewa ya oksijen isilete madhara mwilini ni lazima itumike yote kwa ufanisi kwani ikibaki mwilini inaweza sababisha kutengenezwa kwa free radicals zinazoweza kupelekea mtu kupata



Free radicals ni atoms zenye namba witiri za elektron ambazo zinauwezo wa kuungana na element kama mercury, shaba ( heavy metals ) pamoja na madawa mengine kutengeneza kemikali zinazoweza kusababisha madhara kwenye chembechembe za urithi ( DNA).
Pamoja na uwezekano wa kupelekea saratani, atom hizi zinaweza zikasababisha:

  • Uchovu wa mwili
  • Kuzeeka mapema
  • Matatizo ya akili
  • Ukosefu wa kumbukumbu
  • Kizunguzungu
  • Kichefuchefu

 Miili yetu ina antioxidants ambazo zina uwezo wa kupambana na free radicals lakini mara nyingine free radical zinaweza kuwa nyingi kupita uwezo wa mwili kupambana nazo. Ili kufanya mili yetu iwe na uwezo wa kupambana na molecule hizi inabidi kutumia njia mbadala ambazo zinaweza zikaongeza uwezo wa kupambana na free radicals.
 Njia zinazoweza kutumika ni kutumia vyakula au supplements zenye vitamin A, Vitamin C, vitamin E selenium pamoja na vingine.

VYAKULA ASILIA VYENYE ANTIOXIDANTS
Vyakula vyenye vitamin A, C na E  vina uwezo wa kuzuia free radicals. Pia vyakula hivi vinauwezo wa kuondoa oxygen inayobaki kwenye seli au kwa kitaalam, Oxygen Radical Absorbing Capacity (ORAC) Vyakula hivyo ni pamoja na:

1. ZABIBU 
Ni mojawapo kati ya matunda yenye Oxygen Radical Absorbing Capacity (ORAC)  au uwezo wa kuondoa hewa ya oksijen inayobaki kwenye seli.

spinach zina kiasi kikubwa cha ORAC kwani pamoja na kua na flavonoids ambazo ni antioxidants, pia zina Vitamin A, C na E ambazo zote ni Antioxidants

Ufuta una Vitamin E kwa wingi ambayo ni antioxidant

maharage meusi yanaweza kuzuia kupata saratani ya utumbo mkubwa (colon cancer)
Maharage haya huachwa  kwenye maji kuanzia usiku hadi asubuhi halafu kupikwa siku inayofuata 

ina vitamin C pamoja na kemikali ambazo zinaweza kusaidia mzunguko wa damu uwe mzuri
Inaweza kutumika kwa kuila kama ilivyo, kwenye chai au chakula.

Kahawa ina antioxidant iitwayo flavonoid ambayo ina uwezo wa kuondoa oxygen iliyozidi kwenye seli.
Mpaka sasa imegundulika kwamba kahawa ndiyo yenye kiasi kikubwa zaidi cha antioxidants kuliko vyakula vingine.

Maharage mabichi yana kiasi kikubwa cha antioxidants



Kula kiasi kidogo cha chocolate kwa siku ni njia nzuri ya kupata antioxidants kwani chocolate ina kiasi kikubwa cha flavonoids.
Pia, chocolate ina uwezo mkubwa wa kutibu matatizo ya moyo na
kufanya mzunguko wa damu uende vizuri










Aina zote hizo za vyakula vinapatikana madukani na sokoni, kwa hiyo ni vizuri kuvitumia ili kuboresha afya zetu.

Sources:
http://articles.timesofindia.indiatimes.com
http://www.prevention.com/
http://www.traditional-foods.com/antioxidants
www.webmd.com/













Tuesday, July 16, 2013

USIYOYAFAHAMU KUHUSU SHINIKIZO LA DAMU (Hypertension/high bloodpressure)


Reviewed by: Dr. Chaula Nezaron
                     +255753095035

SHINIKIZO LA DAMU NI NINI?

Ni ugonjwa unaosababisha kuongezeka kwa msukumo wa damu kwenye mishipa inayotoa damukwenye moyo (arteries). Shinikizo la damu ni mojawapo kati ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Ugonjwa huu husababisha  moyo kufanya kazi kwa nguvu Zaidi ya kawaida ili kusukuma damu mwilini. Tatizo la msongo wa damu, pamoja kisukari ni matatizo ambayo yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mtindo wa maisha, na idadi ya watu wanaougua ugonjwa huu imekua ikiongezeka siku hadi siku kutokana na mabadiliko hayo.
Ugonjwa huu ni hatari kwa kuwa mara nyingi hauonyeshi dalili zozote, mpaka mtu anapoanza kuathirika kwa kiasi kikubwa (chronic)

AINA ZA SHINIKIZO LA DAMU (Presha)


  Primary hypertension

Hii ni aina ya presha inayowakumba watu wengi (90-95%) kuliko aina nyingine ya shinikizo la damu, na huwa sababu zinazopelekea aina hii ya shinikizo la damu hazijulikani mpaka sasa.
2    
              Secondary hypertension

Hii ni aina ya shinikizo la damu linalokumba asilimia chache Zaidi (5-10%) ya watu kuliko aina ya kwanza ya shinikizo la damu. Aina hii ya shinikizo la damu unaweza kusababishwa na matatizo kama:
·         Watu watokao kwenye familia zenye historia ya kupata shinikizo la damu wana hatari kubwa Zaidi ya kupata shinikizo la damu kuliko watu watokao kwenye familia zisizo na historia hiyo.

  •  Matatizo ya moyo (Heart failure)


  • Matatizo ya figo (Renal failure)


  •  Matatizo ya mishipa ya damu ( kupungua ukubwa wa mishipa ya damu/atherosclerosis)


  • Unene kupita kiasi (Obesity)


  • Watu wasiofanya mazoezi mara kwa mara wana hatari kubwa Zaidi ya kupata shinikizo la damu

  •  Kutumia chumvi nyingi

  •  Ulevi wa pombe, sigara na dawa za kulevya

  • Magonjwa ya meno


  • ·     Watu wenye umri kati ya miaka 40 na kuendelea wana uwezekano mkubwa Zaidi wa kupata shinikizo la damu.

  

  
Shinikizo la damu wakati wa ujauzito
Imegundulika kwamba asilimia 8-10% ya akina mama wanapata shinikizo la damu wakati wa ujauzito na huchangia asilimia 16% ya vifo vya wajawazito duniani pamoja na kuongeza hatari ya vifo vya watoto wachanga kabla ya kujifungua na hivyo akina mama wanashauriwa wahudhurie kliniki ili wafahamu njia za kujikingA
Wajawazito wenye shinikizo la damu huwa wanaweza wakapata dalili zifuatazo:
  •  Kushindwa kuona vizuri
  •   Kujaa maji kwenye mapafu (pulmonary edema)
  • Miguu kujaa maji ( edema)
  •  Kizunguzungu

SHINIKIZO LA DAMU KWA WATOTO
Dalili za shinikizo la damu kwa watoto
  
  •  Kutokwa na damu puani
·  Matatizo ya macho
·  Mtoto kushindwa kukua vizuri
·  Paralysis

Visababishi vya shinikizo la damu kwa watoto
Watoto wanaweza kupata shinikizo la damu kutokana na sababu zifwatazo:
  • Matumizi ya pombe na sigara wakati wa ujauzito
  •   Kuzaliwa kabla ya siku (premature birth)
  •   Kukosa maziwa ya mama (kutokunyonyesha)

  
JINSI YA KUJIKINGA NA SHINIKIZO LA DAMU
  • Fanya mazoezi mara kawa mara
  •  Punguza matumizi ya chumvi na sukari
  •  Punguza matumizi ya pombe
  •  Kula matunda na mboga mboga kwa wingi
  • Epuka vyakula vyenye mafuta mengi

N.B: Kwa kua mara nyingi kisukari hakina dalili kwa watu wazima, ni muhimu kuhudhuria kwenye kituo cha afya mara kwa mara ili ukapime shinikizo la damu

Kwa akina mama wajawazito:

  •  Epuka pombe na sigara wakati wa ujauzito
  •    Fanya mazoezi mepesi ya mwili wakati wa ujauzito

  •   Hakikisha mtoto anapata maziwa ya mama, na wala siyo maziwa ya makopo

  •   Hudhuria kliniki kipindi chote cha ujauzito kama unavyoelekezwa na wahudumu wa afya.
  • Kama una matatizo ya meno, mwone daktari utibiwe mapema kwani yanaweza kusababisha matatizo ya moyo







MATIBABU


Matibabu ya shinikizo la damu bado hayajapatikana,  lakini dawa za kutuliza zinapatikanatembelea kituo cha afya kilicho karibu nawe kwa ushauri Zaidi.

vyanzo: