Huu ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya dengue (dengue
virus) na kusambazwa na mbu aina ya aedes.
Mpaka sasa ugonjwa wa dengue hauna kinga. Ugonjwa wa dengu unapatikana Zaidi
katika maeneo yenye joto (tropical regions) ambayo mengi yapo karibu na ikweta.
Katika miaka ya karibuni maambukizi ya ugonjwa huu yameongezeka kutokana na
mabadiliko ya tabia nchi, muongezeko wa idadi ya watu pamoja na kuongezeka kwa
safari za nje ya nchi Ugonjwa wa dengue umeenea Zaidi katika nchi za kusini mwa
jangwa la sahara, amerika ya kusini pamoja na asia ya kusini.
JINSI UGONJWA UNAVYOSAMBAZWA
Ugonjwa wa dengue husambazwa na mbu aina ya aedes ambao hupendelea kuishi na kuzaliana
kwenye maji yaliyotuama na mbu hawa hupendelea kuuma nyakati za mchana. Mbu
huweza kusamabaza ugonjwa wa dengu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Ugonjwa huu pia unawezwa kusambazwa kwa njia ya kuongezewa damu ya mtu mwenye dengue, au
kwa kubadilishiwa kiungo cha mtu mwenye dengue (mfano figo)
DALILI ZA HOMA YA DENGUE
Zaidi ya asilimia 80 ya watu walioambukizwa dengue huwa hawaonyeshi
dalili zozote za ugonjwa huu.
Dalili za ugonjwa wa dengu kwa wastani hujitokeza siku 3
hadi siku 14 baada ya kuambukizwa, ila kwa watu walio wengi dalili hujitokeza
siku 4 hadi 7 baada ya kuumwa na mbu mwenye ugonjwa huu.
Dalili za mwanzo za dengue ni pamoja na:
- · Homa
- · Kuharisha na kutapika
- · Mumivu makali ya kichwa
- · Maumivu ya misuli na viungo
- · Uchovu wa mwili
Ugonjwa usipotibiwa mapema Baatdi ya watu pia huweza kupata
dalili ,baya Zaidi kama vile:
- · Kutokwa na damu kwenye sehemu zenye uwazi(puani, mdomoni)
- · Kupungu kazi ya mapigo ya moyo
- · Kupata vipele vyekundu kwenye ngozi (erythema)
- · Damu kushindwa kuganda likitokea jeraha
Ugonjwa wa dengue pia huweza kupeleka matatizo ya moyo,
upungufu wa damu pamoja na matatizo ya ini
Ni rahisi kuzifananisha dalili nyingi za homa ya dengu na
zile za malaria pamoja na mafua hivyo ni vyema ukapime kwanza kabla hujaanza
matibabu ya malaria.
MATIBABU
Tiba ya dengue inalenga kupunguza
dalili za ugonjwa na wala siyo kuangamiza virus vya dengue (symptomatic treatment). Dawa ya maumivu
inayoshauriwa kutumika kutuliza maumivu kwa wenye ugonjwa huu ni PARACETAMOL.
Utafiti uliofanyika nchini India na
kuchapishwa kwenye tovuti ya wizara ya afya ya marekani,
umethibitisha kwamba majani ya mpapai (carica
papaya) yana uwezo wa kutibu ugonjwa wa dengue. Hata hivyo, Dk Vinitah Saini kutoka hospitali ya Muhimbili alisema ingawa baadhi ya maeneo wanatumia juisi ya majani ya mpapai kutibu ugonjwa huo lakini akasema hakuna ushahidi wa kisayansi kuwa yanatibu. Majani hayo hutumika kutengeneza
juisi ambayo hunywewa kama dawa
TAHADHARI
Matumizi ya dawa za maumivu kama
vile ASPIRIN na IBUPROFEN ni hatari kwa mtu mwenye homa ya dengue kwani zinaweza kufanya
hali iwe mbaya Zaidi na kusababisha kifo. Dawa za aspirini pamoja na ibuprofen
husababisha damu nyingi Zaidi kuvuja na hivyo hupelekea upungufu mkubwa Zaidi wa
damu.
JINSI YA KUJIKINGA NA HOMA YA DENGUE
Mbinu za kujikinga na dengue
zinahusisha kujikinga kuumwa na mbu, na nyingi zinafanana na zile za kujikinga
na malaria. Zifuatazo ni baadhi ya njia za kujikinga na homa ya dengue:
- Tokomeza mazalia ya mbu kwa kufukia maji yaliyotuama, ikiwa na pamoja na makopo, vifuu pamoja na vitu vingine vinavyoweza kukinga maji.
- · Lala kwenye chandarua
- Jipake mafuta ya kufukuza mbu
Vyanzo:
No comments:
Post a Comment