Reviewed by: Dr. Chaula Nezaron
+255753095035
SHINIKIZO LA DAMU NI NINI?
Ni
ugonjwa unaosababisha kuongezeka kwa msukumo wa damu kwenye mishipa inayotoa
damukwenye moyo (arteries). Shinikizo
la damu ni mojawapo kati ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Ugonjwa
huu husababisha moyo kufanya kazi kwa
nguvu Zaidi ya kawaida ili kusukuma damu mwilini. Tatizo la msongo wa damu,
pamoja kisukari ni matatizo ambayo yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mtindo wa
maisha, na idadi ya watu wanaougua ugonjwa huu imekua ikiongezeka siku hadi
siku kutokana na mabadiliko hayo.
Ugonjwa
huu ni hatari kwa kuwa mara nyingi hauonyeshi dalili zozote, mpaka mtu
anapoanza kuathirika kwa kiasi kikubwa (chronic)
AINA ZA SHINIKIZO LA DAMU (Presha)
Primary hypertension
Hii ni aina ya presha inayowakumba
watu wengi (90-95%) kuliko aina nyingine ya shinikizo la damu, na huwa sababu
zinazopelekea aina hii ya shinikizo la damu hazijulikani mpaka sasa.
2
Secondary hypertension
Hii ni aina ya
shinikizo la damu linalokumba asilimia chache Zaidi (5-10%) ya watu kuliko aina
ya kwanza ya shinikizo la damu. Aina hii ya shinikizo la damu unaweza
kusababishwa na matatizo kama:
·
Watu watokao
kwenye familia zenye historia ya kupata shinikizo la damu wana hatari kubwa
Zaidi ya kupata shinikizo la damu kuliko watu watokao kwenye familia zisizo na
historia hiyo.
- Matatizo ya figo (Renal failure)
- Matatizo ya mishipa ya damu ( kupungua ukubwa wa mishipa ya damu/atherosclerosis)
- Unene kupita kiasi (Obesity)
- Kutumia chumvi nyingi
- Ulevi wa pombe, sigara na dawa za kulevya
- Magonjwa ya meno
- · Watu wenye umri kati ya miaka 40 na kuendelea wana uwezekano mkubwa Zaidi wa kupata shinikizo la damu.
Shinikizo la
damu wakati wa ujauzito
Imegundulika kwamba
asilimia 8-10% ya akina mama wanapata shinikizo la damu wakati wa ujauzito na huchangia asilimia 16% ya
vifo vya wajawazito duniani pamoja na kuongeza hatari ya vifo vya watoto
wachanga kabla ya kujifungua na hivyo akina mama wanashauriwa wahudhurie
kliniki ili wafahamu njia za kujikingA
Wajawazito wenye
shinikizo la damu huwa wanaweza wakapata dalili zifuatazo:
- Kushindwa kuona vizuri
- Kujaa maji kwenye mapafu (pulmonary edema)
- Miguu kujaa maji ( edema)
- Kizunguzungu
SHINIKIZO LA DAMU KWA WATOTO
Dalili za shinikizo la damu kwa
watoto
· Mtoto kushindwa kukua vizuri
· Paralysis
Visababishi vya
shinikizo la damu kwa watoto
Watoto wanaweza kupata
shinikizo la damu kutokana na sababu zifwatazo:
- Matumizi ya pombe na sigara wakati wa ujauzito
- Kuzaliwa kabla ya siku (premature birth)
- Kukosa maziwa ya mama (kutokunyonyesha)
JINSI YA
KUJIKINGA NA SHINIKIZO LA DAMU
- Fanya mazoezi mara kawa mara
- Punguza matumizi ya chumvi na sukari
- Punguza matumizi ya pombe
- Kula matunda na mboga mboga kwa wingi
- Epuka vyakula vyenye mafuta mengi
N.B: Kwa kua mara nyingi kisukari hakina dalili kwa watu
wazima, ni muhimu kuhudhuria kwenye kituo cha afya mara kwa mara ili ukapime shinikizo
la damu
- Epuka pombe na sigara wakati wa ujauzito
- Fanya mazoezi mepesi ya mwili wakati wa ujauzito
- Hakikisha mtoto anapata maziwa ya mama, na wala siyo maziwa ya makopo
- Hudhuria kliniki kipindi chote cha ujauzito kama unavyoelekezwa na wahudumu wa afya.
- Kama una matatizo ya meno, mwone daktari utibiwe mapema kwani yanaweza kusababisha matatizo ya moyo
MATIBABU
Matibabu ya
shinikizo la damu bado hayajapatikana, lakini dawa za kutuliza zinapatikanatembelea kituo cha afya kilicho karibu nawe kwa
ushauri Zaidi.
vyanzo:
No comments:
Post a Comment